Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 45:3-5,7,8

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

3 Yosefu akawaambia ndugu zake, "Mimi ni Yosefu! Je, baba yangu angali hai bado?" Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.

4 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, "Sogeeni karibu nami." Waliposogea, akasema, "Mimi ni ndugu yenu Yosefu, yule ambaye mlimuuza Misri! 5 Sasa, msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. 7 Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuhifadhi mabaki kwa ajili yenu katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu.

8 "Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kuwa baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    3 Yusufu akawaambia ndugu zake, "Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?" Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.

    4 Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake, "Sogeeni karibu nami." Waliposogea, akasema, "Mimi ni ndugu yenu Yusufu, yule ambaye mlimuuza Misri! 5 Sasa msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. 7 Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuwahifadhia mabaki katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu.

    8 "Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kama baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    3 Mdo 7:13;Mt 14:26;Mk 6:50Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake. 4 Mwa 37:28Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. 5 Isa 40:2;2 Kor 2:7;Mwa 50:20;Kum 23:14;2 Sam 16:10,11;Zab 33:18,19;Mdo 4:24;2 Pet 2:9Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinituma mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. 7 Mungu alinituma mbele yenu kuwahifadhia mabaki katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. 8 Mwa 41:43;Amu 17:10;Ayu 29:16Basi si ninyi mlionileta huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.