3 Yusufu akawaambia ndugu zake, "Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?" Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.
4 Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake, "Sogeeni karibu nami." Waliposogea, akasema, "Mimi ni ndugu yenu Yusufu, yule ambaye mlimuuza Misri! 5 Sasa msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. 7 Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuwahifadhia mabaki katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu.
8 "Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kama baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote.