Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 9:20-25

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

20 Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. 21 Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

24 Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea, 25 akasema,

"Alaaniwe Kanaani!

Atakuwa mtumwa wa chini sana

kuliko watumwa wote kwa ndugu zake."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    20 Nuhu akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. 21 Alipokunywa huo mvinyo wake, akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo, wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

    24 Nuhu alipolevuka na kujua lile mwanawe mdogo alilomtendea, 25 akasema,

    "Alaaniwe Kanaani!

    Atakuwa mtumwa wa chini kabisa

    kwa ndugu zake."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    20 Mwa 3:19;4:2;Mhu 5:9Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; 21 Mwa 19:32,36;Mit 20:1;Efe 5:18akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23 Kut 20:12;Gal 6:1Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

    24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. 25 Kum 27:16;Mt 25:41;Yos 9:23;1 Fal 9:20Akasema,

    Na alaaniwe Kanaani;

    Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.