20 Mwa 3:19;4:2;Mhu 5:9Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; 21 Mwa 19:32,36;Mit 20:1;Efe 5:18akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23 Kut 20:12;Gal 6:1Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. 25 Kum 27:16;Mt 25:41;Yos 9:23;1 Fal 9:20Akasema,
Na alaaniwe Kanaani;
Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.