Pular para o conteúdo
Publicidade

Waebrania 10:1-4

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Dhabihu Ya Kristo Ni Mara Moja Tu

1 Sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. 2 Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. 3 Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, 4 kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kupitia kwa dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. 2 Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. 3 Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, 4 kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Ebr 8:5;7:19Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakaribiao. 2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? 3 Law 16:21Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. 4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.