Pular para o conteúdo
Publicidade

Yona 4:1-4,10,11

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Hasira Ya Yona Kwa Ajili Ya Huruma Ya Bwana.

1 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. 2 Akamwomba Bwana, "Ee Bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. 3 Sasa, Ee Bwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi."

4 Lakini Bwana akamjibu, "Je unayo haki yoyote kukasirika?"

10 Lakini Bwana akamwambia, "Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja. 11 Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?"

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. 2 Akamwomba Mwenyezi Mungu, "Ee Mwenyezi Mungu, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharakisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. 3 Sasa, Ee Mwenyezi Mungu, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi."

    4 Lakini Mwenyezi Mungu akamjibu, "Je unayo haki yoyote kukasirika?"

    10 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, "Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja. 11 Lakini Ninawi ina zaidi ya watu elfu mia moja na ishirini ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ng’ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri kuhusu mji ule mkubwa?"

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mt 20:15Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika. 2 Kut 34:6Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nilijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. 3 1 Fal 19:4Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi. 4 Naye BWANA akasema, Je! Unatenda vema kukasirika?

    10 Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; 11 Eze 33:11;Kum 1:39;Zab 36:6na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya elfu mia moja na ishirini, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Jonas
Ver todos os capítulos de Jonas