Hasira ya Yona kwa ajili ya huruma ya Mwenyezi Mungu
1 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. 2 Akamwomba Mwenyezi Mungu, "Ee Mwenyezi Mungu, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharakisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. 3 Sasa, Ee Mwenyezi Mungu, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi."
4 Lakini Mwenyezi Mungu akamjibu, "Je unayo haki yoyote kukasirika?"
10 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, "Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja. 11 Lakini Ninawi ina zaidi ya watu elfu mia moja na ishirini ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ng’ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri kuhusu mji ule mkubwa?"