Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 10:3-5,14,27

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

3 Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 4 Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake. 5 Lakini kondoo hawatamfuata mgeni bali watamkimbia, kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni."

14 "Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua.

27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata,

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    3 Mlinzi humfungulia lango, na kondoo huisikia sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 4 Baada ya kuwatoa wote nje, yeye hutangulia mbele yao na kondoo humfuata, kwa kuwa wanaijua sauti yake. 5 Lakini kondoo hawatamfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni."

    14 "Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu, nao kondoo wangu wananijua.

    27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Yn 10:27Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

    14 2 Tim 2:19Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;

    27 Yn 8:47;10:3,4Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.