3 Mlinzi humfungulia lango, na kondoo huisikia sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 4 Baada ya kuwatoa wote nje, yeye hutangulia mbele yao na kondoo humfuata, kwa kuwa wanaijua sauti yake. 5 Lakini kondoo hawatamfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni."
14 "Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu, nao kondoo wangu wananijua.
27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata.