14 Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi.
Pilato akawaambia Wayahudi, "Huyu hapa mfalme wenu!"
29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachovya sifongo kwenye hiyo siki, wakaiweka kwenye ufito wa mti wa hisopo, wakampelekea mdomoni.
33 Lakini walipomkaribia Yesu, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake. 36 Kwa maana mambo haya yalitukia ili Maandiko yapate kutimia, yale yasemayo, "Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa."