Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 19:23-27

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Mavazi Ya Yesu Yagawanywa

23 Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini. 24 Wakaambiana, "Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani atalichukua."

Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema,

"Wanagawana nguo zangu,

na vazi langu wanalipigia kura."

Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari.

25 Wakati huo huo karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Maria mke wa Klopa, na Maria Magdalene. 26 Yesu alipomwona mama yake mahali pale pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, akamwambia mama yake, "Mwanamke, huyo hapo ndiye mwanao," 27 kisha akamwambia yule mwanafunzi, "Nawe huyo hapo ndiye mama yako." Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.

Kifo Cha Yesu

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49)

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    23 Askari walipokwisha kumsulubisha Isa, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono, bali limefumwa tangu juu hadi chini.

    24 Wakaambiana, "Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani atalichukua."

    Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema,

    "Wanagawana nguo zangu,

    na vazi langu wanalipigia kura."

    Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari.

    25 Karibu na msalaba wa Isa walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Mariamu mke wa Klopa, na Mariamu Magdalene. 26 Isa alipomwona mama yake mahali pale, na yule mwanafunzi aliyempenda akiwa amesimama karibu, Isa akamwambia mama yake, "Mama, huyu hapa ndiye mwanao." 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, "Nawe huyu hapa ndiye mama yako." Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Isa nyumbani mwake.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    23 Nao askari walipomsulubisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. 24 Zab 22:18Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo,

    Waligawanya nguo zangu,

    Na vazi langu wakalipigia kura.

    Basi ndivyo walivyofanya wale askari.

    25 Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. 26 Yn 13:23Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.