26 Yesu alipomwona mama yake mahali pale pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, akamwambia mama yake, "Mwanamke, huyo hapo ndiye mwanao," 27 kisha akamwambia yule mwanafunzi, "Nawe huyo hapo ndiye mama yako." Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.
Kifo Cha Yesu
(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49)
28 Baada ya haya, Yesu hali akijua kuwa mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, "Naona kiu." 30 Baada ya kuionja hiyo siki, Yesu akasema, "Imekwisha." Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake.