Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 19:26-28,30

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

26 Isa alipomwona mama yake mahali pale, na yule mwanafunzi aliyempenda akiwa amesimama karibu, Isa akamwambia mama yake, "Mama, huyu hapa ndiye mwanao." 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, "Nawe huyu hapa ndiye mama yako." Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Isa nyumbani mwake.

Kifo cha Isa

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49)

28 Baada ya haya, akijua kuwa mambo yote yamemalizika, na ili kutimiza Maandiko, Isa akasema, "Naona kiu." 30 Baada ya kuionja hiyo siki, Isa akasema, "Imekwisha." Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    26 Yn 13:23Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.

    28 Zab 22:15;69:21;Yn 13:3;18:4Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu. 30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    26 Yesu alipomwona mama yake mahali pale pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, akamwambia mama yake, "Mwanamke, huyo hapo ndiye mwanao," 27 kisha akamwambia yule mwanafunzi, "Nawe huyo hapo ndiye mama yako." Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.

    28 Baada ya haya, Yesu hali akijua kuwa mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, "Naona kiu." 30 Baada ya kuionja hiyo siki, Yesu akasema, "Imekwisha." Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.