6 Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.2:6 Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40; hivyo kila mtungi ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120.
7 Yesu akawaambia wale watumishi, "Ijazeni hiyo mitungi maji." Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu.
8 Kisha akawaambia, "Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza."
Hivyo wakachota, wakampelekea.