Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 2:6-8

SRUV Swahili Revised Union Version

6 Mk 7:3,4Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza mpaka juu. 8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    6 Basi hapo palikuwa na mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe; iliwekwa hapo kwa ajili ya desturi ya Kiyahudi ya kujitakasa; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu2:6 Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40..

    7 Isa akawaambia wale watumishi, "Ijazeni hiyo mitungi maji." Nao wakaijaza ile mitungi hadi juu.

    8 Kisha akawaambia, "Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe."

    Hivyo wakachota, wakampelekea.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    6 Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.2:6 Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40; hivyo kila mtungi ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120.

    7 Yesu akawaambia wale watumishi, "Ijazeni hiyo mitungi maji." Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu.

    8 Kisha akawaambia, "Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza."

    Hivyo wakachota, wakampelekea.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.