Kufufuka Kwa Yesu
1 Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.
11 Lakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini,
14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.
16 Yesu akamwita, "Maria!"
Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, "Rabboni!" (maana yake Mwalimu).
17 Yesu akamwambia, "Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ "
18 Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, "Nimemwona Bwana!" Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.
Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49)