Isa afufuka
1 Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa bado giza, Mariamu Magdalene alienda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.
11 Lakini Mariamu Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama kuchungulia mle kaburini,
14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Isa amesimama, lakini hakumtambua.
16 Isa akamwita, "Mariamu!"
Ndipo Mariamu akamgeukia Isa na kusema naye kwa Kiebrania, "Raboni!" (maana yake "Mwalimu").
17 Isa akamwambia, "Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba20:17 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili.. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ "
18 Kwa hiyo Mariamu Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Isa, akisema, "Nimemwona Bwana!" Naye akawaambia kwamba Isa alikuwa amemweleza mambo hayo yote.
Isa awatokea wanafunzi wake
(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49)