Pular para o conteúdo
Publicidade

Yeremia 18:2-6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

2 "Shuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu." 3 Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. 4 Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kama vile ilivyoonekana vyema kwake yeye.

5 Kisha neno la Bwana likanijia kusema: 6 "Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?" asema Bwana. "Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 "Shuka uende hadi nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu." 3 Kwa hiyo nikashuka hadi nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. 4 Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake; hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kwa namna alivyoona ni vyema machoni pake.

    5 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: 6 "Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?" asema Mwenyezi Mungu. "Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    2 Ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha maneno yangu. 3 Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na tazama, alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu. 4 Rum 11:15Na chombo kile, alichokuwa akikifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikitengeneza tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya.

    5 Ndipo neno la BWANA likanijia, kusema, 6 Isa 45:9;64:8Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema BWANA. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.