14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa!
Nayo isibarikiwe ile siku
mama yangu aliyonizaa!
15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,
yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,
"Mtoto amezaliwa kwako,
tena mtoto wa kiume!"
16 Mtu huyo na awe kama miji ile
ambayo Bwana Mungu
aliiangamiza bila huruma.
Yeye na asikie maombolezo asubuhi
na kilio cha vita adhuhuri.
17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,
hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,
nalo tumbo lake la uzazi
lingebaki kuwa kubwa daima.
18 Kwa nini basi nilitoka tumboni
ili kuona taabu na huzuni,
na kuzimaliza siku zangu katika aibu?