Pular para o conteúdo
Publicidade

Jeremias 31

31 "Siku zinakuja," asema Bwana,

"nitakapofanya agano jipya

na nyumba ya Israeli

na nyumba ya Yuda.

32 Halitafanana na agano

nililofanya na baba zao

wakati nilipowashika mkono

kuwaongoza watoke Misri,

kwa sababu walivunja agano langu,

ijapokuwa nilikuwa mume kwao,"

asema Bwana.

33 "Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli

baada ya siku zile," asema Bwana.

"Nitaweka sheria yangu katika nia zao,

na kuiandika mioyoni mwao.

Nitakuwa Mungu wao,

nao watakuwa watu wangu.

Veja também