Pular para o conteúdo
Publicidade

Yeremia 31:32-34

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

32 Halitafanana na agano

nililofanya na baba zao

wakati nilipowashika mkono

kuwaongoza watoke Misri,

kwa sababu walivunja agano langu,

ijapokuwa nilikuwa mume kwao,"

asema Bwana.

33 "Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli

baada ya siku zile," asema Bwana.

"Nitaweka sheria yangu katika nia zao,

na kuiandika mioyoni mwao.

Nitakuwa Mungu wao,

nao watakuwa watu wangu.

34 Mtu hatamfundisha tena jirani yake,

wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’

kwa sababu wote watanijua mimi,

tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,"

asema Bwana.

"Kwa sababu nitasamehe uovu wao,

wala sitazikumbuka dhambi zao tena."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    32 Halitafanana na agano

    nililofanya na baba zao

    wakati nilipowashika mkono

    kuwaongoza watoke Misri,

    kwa sababu walivunja agano langu,

    ijapokuwa nilikuwa mume kwao,"

    asema Mwenyezi Mungu.

    33 "Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli

    baada ya siku zile," asema Mwenyezi Mungu.

    "Nitaweka sheria yangu katika nia zao,

    na kuiandika mioyoni mwao.

    Nitakuwa Mungu wao,

    nao watakuwa watu wangu.

    34 Mtu hatamfundisha tena jirani yake,

    wala mtu kumfundisha ndugu yake, akisema,

    ‘Mjue Mwenyezi Mungu,’

    kwa sababu wote watanijua mimi,

    kuanzia aliye mdogo hata aliye mkubwa kuliko wote,"

    asema Mwenyezi Mungu.

    "Nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    32 Yn 1:17;Kum 1:31Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nilikuwa mume kwao, asema BWANA. 33 Yer 32:40;24:7;30:22;Zab 40:8;2 Kor 3:3;Ebr 10:16Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 34 Isa 54:13;Yn 6:45;1 Kor 2:10;Yer 33:8;Rum 11:27;Ebr 10:17Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.