16 Ndipo hao watu wakajibu, "Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Bwana na kuitumikia miungu mingine! 17 Bwana Mungu wetu mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao.
Publicidade
Publicidade