Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 17:3-6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

3 Kwa hiyo, jilindeni.

"Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu, msamehe. 4 Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe."

Imani

5 Mitume wake wakamwambia Bwana, "Tuongezee imani."

6 Bwana akawajibu, "Kama mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ngʼoka ukaote baharini,’ nao ungewatii.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    3 Kwa hiyo, jilindeni.

    "Ndugu yako akikukosea, mwonye; naye akitubu, msamehe. 4 Akikukosea mara saba kwa siku moja, na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe."

    5 Mitume wake wakamwambia Bwana, "Tuongezee imani."

    6 Bwana akawajibu, "Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    3 Mt 18:15Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. 4 Mt 18:21,22Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

    5 Mk 9:24Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. 6 Mt 17:20;21:21Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.