3 Kwa hiyo, jilindeni.
"Ndugu yako akikukosea, mwonye; naye akitubu, msamehe. 4 Akikukosea mara saba kwa siku moja, na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe."
Imani
5 Mitume wake wakamwambia Bwana, "Tuongezee imani."
6 Bwana akawajibu, "Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.