34 Yesu akasema, "Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!" Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
43 Yesu akamjibu, "Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso."23:43 Paradiso maana yake bustani nzuri, hapa ina maana mahali zinapokwenda roho za wacha Mungu, yaani watakatifu.
Kifo Cha Yesu
(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30)
46 Yesu akapaza sauti yake akasema, "Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu." Baada ya kusema haya, akakata roho.