Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 5:12,13

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

12 Ikawa siku moja Yesu alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Yesu, alianguka chini mpaka uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, "Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa."

13 Yesu akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, "Nataka. Takasika!" Na mara ukoma wake ukatakasika.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Ikawa siku moja Isa alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Isa, alianguka chini hadi uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, "Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa."

    13 Isa akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, "Nataka. Takasika!" Na mara ukoma wake ukatakasika.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    12 Mt 8:1-4;Mk 1:40-45Ikawa, alipokuwa katika mmojawapo wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejaa ukoma; naye alipomwona Yesu alianguka kifudifudi, akamwomba akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 13 Naye akaunyosha mkono wake, akamgusa akisema, Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukamwondoka.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.