Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 8:43-48

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

43 Katika umati huo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna yeyote aliyeweza kumponya. 44 Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Yesu na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma.

45 Yesu akauliza, "Ni nani aliyenigusa?"

Watu wote walipokana, Petro akasema, "Bwana, huu umati wa watu unakusonga na kukusukuma kila upande."

46 Lakini Yesu akasema, "Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka."

47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Yesu. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara. 48 Basi Yesu akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    43 Palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, [na alikuwa amegharimia mali yake yote kwa matibabu]8:43 Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya. lakini hakuna yeyote aliyeweza kumponya. 44 Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Isa na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma.

    45 Isa akauliza, "Ni nani aliyenigusa?"

    Watu wote walipokana, Petro akasema, "Bwana, umati huu wa watu wanakusonga na kukusukuma kila upande."

    46 Lakini Isa akasema, "Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka."

    47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara moja. 48 Basi Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu yeyote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. 45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. 46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka. 47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara moja. 48 Lk 7:50Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya; nenda zako na amani.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.