43 Palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, [na alikuwa amegharimia mali yake yote kwa matibabu]8:43 Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya. lakini hakuna yeyote aliyeweza kumponya. 44 Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Isa na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma.
45 Isa akauliza, "Ni nani aliyenigusa?"
Watu wote walipokana, Petro akasema, "Bwana, umati huu wa watu wanakusonga na kukusukuma kila upande."
46 Lakini Isa akasema, "Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka."
47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara moja. 48 Basi Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."