Pular para o conteúdo
Publicidade

Mambo Ya Walawi 24:5-9

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

5 "Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa24:5 Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo mbili. za unga kwa kila mkate. 6 Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. 7 Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto. 8 Mikate hii itawekwa mbele za Bwana kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu. 9 Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    5 "Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi ya efa24:5 Sehemu mbili za kumi ya efa ni sawa na kilo mbili. ya unga kwa kila mkate. 6 Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Mwenyezi Mungu juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. 7 Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto. 8 Mikate hii itawekwa mbele za Mwenyezi Mungu kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa agano la kudumu. 9 Hii ni mali ya Haruni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao milele la sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    5 Kut 25:30;40:24Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja. 6 1 Fal 7:48;2 Nya 4:19;Ebr 9:2Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za BWANA. 7 Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto. 8 Hes 4:7;1 Nya 9:32;2 Nya 2:4Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za BWANA daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele. 9 Mt 12:4;Mk 2:26;Lk 6:4;1 Sam 21:6;Kut 29:33;Law 8:3;21:22Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zitolewazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.