Mikate ya Hema Takatifu
5 Kut 25:30;40:24Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja. 6 1 Fal 7:48;2 Nya 4:19;Ebr 9:2Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za BWANA. 7 Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto. 8 Hes 4:7;1 Nya 9:32;2 Nya 2:4Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za BWANA daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele. 9 Mt 12:4;Mk 2:26;Lk 6:4;1 Sam 21:6;Kut 29:33;Law 8:3;21:22Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zitolewazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.