6 Yesu akawajibu, "Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa:
" ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,
lakini mioyo yao iko mbali nami.
7 Huniabudu bure,
nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’
8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu."