Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 9:17,25-27

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

17 Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.

25 Yesu alipoona kwamba umati wa watu unakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, "Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!"

26 Yule pepo mchafu akiisha kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, na akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, "Amekufa." 27 Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    17 Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.

    25 Isa alipoona kwamba umati wa watu wanakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, "Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!"

    26 Baada ya yule pepo mchafu kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, "Amekufa." 27 Lakini Isa akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    17 Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; 25 Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. 26 Mk 1:26Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. 27 Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.