17 Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.
25 Isa alipoona kwamba umati wa watu wanakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, "Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!"
26 Baada ya yule pepo mchafu kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, "Amekufa." 27 Lakini Isa akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.