25 Wakati wa zamu ya nne ya usiku,14:25 Zamu ya nne ya usiku ni kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi. Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26 Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, "Ni mzimu." Wakapiga yowe kwa kuogopa.
27 Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope."