24 Yesu akajibu, "Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea."
25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu, akasema, "Bwana, nisaidie!"
26 Yesu akajibu, "Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
27 Yule mwanamke akajibu, "Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao."
28 Ndipo Yesu akamwambia, "Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka." Naye binti yake akapona tangu saa ile.