Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 15:24-28

SRUV Swahili Revised Union Version

24 Mt 10:6Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. 26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 28 Mt 8:10,13Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    24 Isa akajibu, "Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea."

    25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Isa, akasema, "Bwana, nisaidie!"

    26 Isa akajibu, "Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."

    27 Yule mwanamke akajibu, "Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwa meza za bwana zao."

    28 Ndipo Isa akamwambia, "Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka." Naye binti yake akapona tangu saa ile.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    24 Yesu akajibu, "Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea."

    25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu, akasema, "Bwana, nisaidie!"

    26 Yesu akajibu, "Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."

    27 Yule mwanamke akajibu, "Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao."

    28 Ndipo Yesu akamwambia, "Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka." Naye binti yake akapona tangu saa ile.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.