3 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, "Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?"
7 Wakamuuliza, "Kwa nini basi Mose aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?"
8 Yesu akawajibu, "Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. 9 Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini."