3 Baadhi ya Mafarisayo19:3 Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli. wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, "Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?"
7 Wakamuuliza, "Kwa nini basi Musa aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?"
8 Isa akawajibu, "Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. 9 Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini."