10 Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, "Huyu ni nani?"
11 Ule umati wa watu ukajibu, "Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya."
Yesu Atakasa Hekalu
(Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)
12 Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13 Akawaambia, "Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi."