10 Isa alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, "Huyu ni nani?"
11 Wale umati wa watu wakajibu, "Huyu ni Isa, yule nabii kutoka Nasiri ya Galilaya."
Isa atakasa Hekalu
(Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)
12 Isa akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13 Akawaambia, "Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi."