Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 21:23-27

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

23 Yesu alipoingia Hekaluni, viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakamjia alipokuwa anafundisha na kusema, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?"

24 Yesu akawajibu, "Nami nitawauliza swali moja. Kama mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25 Ubatizo wa Yohana, ulitoka wapi? Je, ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?"

Wakahojiana wao kwa wao na kusema, "Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 26 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii."

27 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, "Sisi hatujui."

Naye akawaambia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    23 Isa alipoingia Hekaluni, viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakamjia alipokuwa anafundisha, wakamuuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?"

    24 Isa akawajibu, "Nami nitawauliza swali moja. Mkinijibu, nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25 Je, ubatizo wa Yahya ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?"

    Wakahojiana wao kwa wao na kusema, "Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 26 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yahya kuwa ni nabii."

    27 Hivyo basi wakamjibu Isa, "Sisi hatujui."

    Naye akawaambia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    23 Mk 11:27-33;Lk 20:1-8Na alipokwisha kuingia hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii?Yn 2:1824 Yesu akajibu akawaambia, Na mimi nitawauliza neno moja; ambalo mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa amri gani ninatenda haya. 25 Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mbona basi hamkumwamini? 26 Mt 14:5Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii. 27 Wakamjibu Yesu wakasema, Hatujui. Naye akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda haya.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.