23 Isa alipoingia Hekaluni, viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakamjia alipokuwa anafundisha, wakamuuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?"
24 Isa akawajibu, "Nami nitawauliza swali moja. Mkinijibu, nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25 Je, ubatizo wa Yahya ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?"
Wakahojiana wao kwa wao na kusema, "Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 26 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yahya kuwa ni nabii."
27 Hivyo basi wakamjibu Isa, "Sisi hatujui."
Naye akawaambia, "Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.