Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 22:17-21

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

17 Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?"

18 Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, "Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi." Wakamletea dinari. 20 Naye akawauliza, "Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?"

21 Wakamjibu, "Ni vya Kaisari."

Basi Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    17 Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?"

    18 Lakini Isa alifahamu kusudi lao mbaya, akawaambia, "Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi." Wakamletea dinari. 20 Naye akawauliza, "Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?"

    21 Wakamjibu, "Ni vya Kaisari."

    Basi Isa akawaambia, "Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    17 Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo? 18 Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? 19 Nionesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. 20 Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii? 21 Rum 13:7Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.