3 Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 4 Akasema, "Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia."
Wakamjibu, "Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako."
5 Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga.
6 Wale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, "Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu." 7 Kwa hiyo baada ya kushauriana, waliamua kuzitumia kununulia shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni.