Yuda ajinyonga
3 Mdo 1:18-19;Mt 26:15Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nilikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. 4 Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe. 5 Mdo 1:18;2 Sam 17:23Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga. 6 Mk 12:41Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni fedha ya damu. 7 Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.