Publicidade

Mateus 9

2 Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Yesu alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, "Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa."

3 Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa sheria wakasema mioyoni mwao, "Huyu mtu anakufuru!"

4 Lakini Yesu akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, "Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, Umesamehewa dhambi zako,au kusema, Inuka, uende? 6 Lakini, ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi" Ndipo akamwambia yule aliyepooza, "Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako." 7 Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani kwake.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-