Publicidade

Salmos 127

Bila Mungu, Kazi Ya Mwanadamu Haifai
Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni.

1 Bwana asipoijenga nyumba,

wajengao hufanya kazi bure.

Bwana asipoulinda mji,

walinzi wakesha bure.

2 Mnajisumbua bure kuamka mapema

na kuchelewa kulala,

mkitaabikia chakula:

kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.

3 Wana ni urithi utokao kwa Bwana,

watoto ni zawadi kutoka kwake.

4 Kama mishale mikononi mwa shujaa

ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

5 Heri mtu ambaye podo lake

limejazwa nao.

Hawataaibishwa wanaposhindana

na adui zao langoni.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-