Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 120

Kuomba Msaada

Wimbo wa kwenda juu.

1 Katika dhiki yangu namwita Bwana,

naye hunijibu.

2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo

na ndimi za udanganyifu.

3 Atakufanyia nini,

au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?

4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,

kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.

5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,

kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!

6 Nimeishi muda mrefu mno

miongoni mwa wale wanaochukia amani.

7 Mimi ni mtu wa amani;

lakini ninaposema, wao wanataka vita.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também