Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 82

Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki

Zaburi ya Asafu.

1 Mungu anaongoza kusanyiko kuu,

anatoa hukumu miongoni mwa "miungu":

2 "Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki

na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

3 Teteeni wanyonge na yatima,

tunzeni haki za maskini na walioonewa.

4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji,

wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

5 "Hawajui lolote, hawaelewi lolote.

Wanatembea gizani;

misingi yote ya dunia imetikisika.

6 "Nilisema, Ninyi ni "miungu";

ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.

7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;

mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote."

8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,

kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também