Publicidade

Salmos 20

Maombi Kwa Ajili Ya Ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki,

jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

2 Na akutumie msaada kutoka patakatifu

na akupatie msaada kutoka Sayuni.

3 Na azikumbuke dhabihu zako zote,

na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.

4 Na akujalie haja ya moyo wako,

na aifanikishe mipango yako yote.

5 Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda,

tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu.

Bwana na akupe haja zako zote.

6 Sasa nafahamu kuwa Bwana

humwokoa mpakwa mafuta wake,

humjibu kutoka mbingu yake takatifu

kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.

7 Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi,

bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.

8 Wao wameshushwa chini na kuanguka,

bali sisi tunainuka na kusimama imara.

9 Ee Bwana, mwokoe mfalme!

Tujibu tunapokuita!

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-